• HABARI MPYA

  Sunday, October 31, 2021

  DK MSOLLA AENGULIWA UCHAGUZI BODI SABABU YA VYETI


  MWENYEKITI wa klabu ya Yanga, Dk Mshindo Mbette Msolla ameenguliwa kwenye uchaguzi wa Bodi ya Ligi Tanzania kwa kile kilichoelezwa hajakidhi vigezo kanuni ya 9 (7) ya vigezo vya kanuni za uchaguzi za TFF toleo la 2021.
  Kwa mujibu wa taarifa ya TFF, Msolla Msolla ameenguliwa kwa kutowasilisha nakala halisi za vyeti vya Taaluma, wakati Mwenyekiti wa Simba SC, Murtaza Ally Mangungu hakuhudhuria usaili.
  Mwenyekiti wa sasa Bodi, Steven Jarvis Mnguto wa Coastal Union ndio mgombea pekee aliyeitishwa kwenye nafasi hiyo kuelekea uchaguzi huo utakaofanyika Novemba 27, mwaka huu mkoani Kigoma, huku Mwenyekiti wa Azam FC, Nassor Idrisa ‘Father’ pekee akipitishwa kugombea nafasi ya Makamu.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DK MSOLLA AENGULIWA UCHAGUZI BODI SABABU YA VYETI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top