• HABARI MPYA

  Thursday, October 21, 2021

  WACHEZAJI YANGA WAMZIKA BABA YAKE BOXER


  WACHEZAJI wa Yanga jana wameshiriki mazishi ya baba wa mchezaji mwenzao, Paul Godfrey Nyang'anya  'Boxer' aliyefariki Dunia Jumatatu Jijini Dar es Salaam.
  Msiba huo ulitokea wakati Boxer, beki wa kulia akiwa Songea mkoani Ruvuma na timu kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya KMC uliofanyika Jumanne na Yanga ikashinda 2-0 Uwanja wa Maji Maji.  Na baada ya timu kurejea tu Dar es Salaam Jumatano msafara ukaenda hospitali ya Temeke kuuga mwili wa marehemu kabla ya mazishi jioni yake. Mungu ampumzishe kwa amani marehemu. Amin.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WACHEZAJI YANGA WAMZIKA BABA YAKE BOXER Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top