• HABARI MPYA

  Wednesday, October 20, 2021

  MESSI AING’ARISHA PSG LIGI YA MABINGWA


  WENYEJI, Paris Saint-Germain wameibuka na ushindi wa 3-2 dhidi ya RB Leipzig katika mchezo wa Kundi A Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Parc des Princes Jijini Paris, Ufaransa.
  Nyota wa mchezo alikuwa ni mshambuliaji Muargentina, Lionel Messi aliyefunga mabao mawili dakika ya 67 na lingine 74 kwa penalti  ya panenka baada ya Kylian Mbappe kufunga la kwanza dakika ya tisa.
  Mabao ya RB Leipzig yalifungwa na Andre Silva dakika ya 28 na Nordi Mukiele dakika ya 57 na kwa ushindi huo PSG inarejea kileleni ikifikisha pointi saba, moja zaidi ya Manchester City baada ya wote kucheza mechi tatu.
  RB Leipzig imefungwa mechi zote tatu na inashika mkia mbele ya Club Brugge yenye pointi nne.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MESSI AING’ARISHA PSG LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top