• HABARI MPYA

  Saturday, October 30, 2021

  MCHEZAJI WA ZAMANI WA SIMBA AFARIKI DUNIA


  MCHEZAJI wa zamani wa Simba SC, Akilimali Yahya, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumamosi ya Oktoba 30, 2021 katika Hospital ya Maweni, Kigoma.
  Winga huyo aliyecheza Simba SC kuanzia mwaka 2003 hadi 2008 anatarajiwa kuzikwa jioni ya leo nyumbani kwao Ujiji Kigoma.
  Baada ya kucheza Simba SC kati ya 2003 na 2008, Akilimali aliyezaliwa Desemba 5, mwaka 1986 alikwenda Mtibwa Sugar ambako alicheza hadi 2010 alipohamia JKT Tanzania alikocheza kwa msimu mmoja akahamia  Coastal Union ya Tanga kabla ya kustaafu soka ya ushindani.
  Mungu ampumzishe kwa amani. Amin.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MCHEZAJI WA ZAMANI WA SIMBA AFARIKI DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top