• HABARI MPYA

  Saturday, October 09, 2021

  TWIGA STARS MABINGWA COSAFA 2021


  TIMU ya taifa ya wanawake ya Tanzania, Twiga Stars imefanikiwa kutwaa ubingwa wa COSAFA baada ya kuichapa Malawi 1-0 jioni ya leo Uwanja wa Nelson Mandela Bay Jijini Port Elizabeth nchini Afrika Kusini.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee la Twiga Stars, Enekia Kasonga dakika ya 64, mchezaji wa Alliance ya Mwanza ambaye hivi karibuni klabu yake imeripotiwa kumuuza Morocco.
  Baada ya mchezo huo, Tuzo ya mchezaji bora wa mchezo huo, Nahodha wa Twiga Stars Amina Bilal alipewa tuzo ya Mchezaji Bora wa kwa mara ya pili mfululizo na kuchaguliwa Mchezaji Bora wa mashindano hayo.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TWIGA STARS MABINGWA COSAFA 2021 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top