• HABARI MPYA

  Tuesday, October 19, 2021

  AZAM FC YAPATA USHINDI WA KWANZA LIGI KUU


  TIMU ya Azam FC imepata ushindi wa kwanza katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu huu baada ya kuichapa Namungo FC 1-0 usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Ni bao la mshambuliaji kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Idris Mbombo dakika ya 90 lililompa pointi tatu za kwanza kocha Mzambia, George Lwandamina leo.
  Azam FC inafikisha pointi nne katika mchezo wa tatu, ikitoka kutoa sare ya 1-1 na Coastal Union Jijini Tanga kabla ya kuchapwa 2-1 na Polisi Tanzania mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, wakati Namungo FC inabaki na pointi tano kufuatia ushindi wa 2-0 dhidi ya Geita Gold kwenye mechi ya kwanza kabla ya sare ya 1-1 na Kagera Sugar zote Uwanja Ilulu mjini Lindi. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAPATA USHINDI WA KWANZA LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top