• HABARI MPYA

  Sunday, October 24, 2021

  POLISI YAICHAPA RUVU SHOOTING 1-0 MLANDIZI


  BAO pekee la mshambuliaji Vitalis Mayanga dakika ya 78, limeipa Polisi Tanzania ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
  Ushindi huo unaifanya Polisi ifikishe pointi tisa baada ya kucheza mechi tatu na sasa inalingana kila kitu na vigogo, Yanga SC wanaoongoza Ligi, wakati Ruvu Shooting inabaki na pointi zake sita za mechi nne sasa katika nafasi ya nne.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: POLISI YAICHAPA RUVU SHOOTING 1-0 MLANDIZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top