• HABARI MPYA

  Thursday, October 21, 2021

  MZAMBIA AIPIGIA ZOTE NNE LEICESTER URUSI


  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Zambia, Patson Daka Jumatano amefunga mabao yote manne kuiwezesha Leicester  City kushinda 4-3 dhidi ya wenyeji, Spartak Moscow katika mchezo wa Kundi C Europe League Uwanja wa Otkrytiye Arena Jijiji Moscow, Urusi.
  Daka mwenye umri wa miaka 23 alifunga mabao hayo dakika za 45,48, 54 na 78, wakati mabao ya Spartak Moscow yalifungwa na Aleksandr Sobolev dakika ya 11 na 86 na Carl Henrik Jordan Larsson dakika ya 44.
  Kwa matokeo hayo, Leicester City inafikisha pointi nne na kusogea nafasi ya pili ikizidiwa pointi mbili na vinara, Legia Warsaw baada ya mechi tatu za awali. 
  Spartak Moscow inabaki nafasi ya tatu na pointi zake tatu mbele ya Napoli yenye pointi moja.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MZAMBIA AIPIGIA ZOTE NNE LEICESTER URUSI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top