• HABARI MPYA

  Wednesday, October 20, 2021

  REAL YAAMKA, YASHINDA 5-0 UGENINI


  TIMU ya Real Madrid imezinduka na kuwatandika wenyeji, Shakhtar Donetsk mabao 5-0 katika mchezo wa Kundi D Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa NSK Olimpiki Jijini Kiev, Ukraine.
  Mabao ya Real Madrid yalifungwa na Serhiy Kryvtsov aliyejifunga dakika ya 37, Vinicius Junior dakika ya 51 na 56, Rodrygo dakika ya 64 na Karim Benzema dakika ya 90.
  Real Madrid inafikisha pointi sita sawa na Sheriff inayoongoza kwa wastani wa mabao, wakifuatiwa na Inter Milan pointi nne na Shakhtar Donets pointi moja baada ya wote kucheza mechi tatu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: REAL YAAMKA, YASHINDA 5-0 UGENINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top