• HABARI MPYA

  Wednesday, October 27, 2021

  WASHELISHELI KUCHEZESHA STARS NA DRC DAR


  KUELEKEA mchezo wa Kundi J kufuzu Fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limetaja waamuzi wa mechi hiyo itakayopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam Novemba 11, mwaka huu.
  Marefa hao ni Camille Bernard atakayepuliza kipyenga, akisaidiwa na washika vibendera Petrousse Henseley, Marie Steve, mezani Fred Emile wote wa Shelisheli.
  Maafisa wengine katika mchezo huo ni Gahungu Desire wa Burundi (Mtathmini Waamuzi), Xaba Simphiwe wa Afrika Kusini (Kamisaa) na Dk Lupondo Violet wa hapa hapa, Tanzania (Daktari).
  Kuelekea mechi mbili za mwisho, Taifa Stars inaongoza kundi hili kwa pointi zake saba, ikiizidi mabao ya kufunga tu Benin, wakifuatiwa na DRC pointi tano na Madagascar pointi tatu baada ya mechi nne.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WASHELISHELI KUCHEZESHA STARS NA DRC DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top