• HABARI MPYA

  Wednesday, October 27, 2021

  CHELSEA YAITOA SOUTHAMPTON KWA MATUTA


  WENYEJI, Chelsea wamefanikiwa kutinga Robo Fainali ya Kombe la Ligi England baada ya ushindi wa penalti 5-4 dhidi ya Southampton kufuatia sare ya 1-1 usi wa Jumanne Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London.

  Kai Havertz alianza kuifungia Chelsea dakika ya 44, kabla ya Che Adams kuisawazishia Southampton dakika ya 47.
  Katika mikwaju ya penalti, kipa 
  Kepa Arrizabalaga aliokoa penalti ya Theo Walcott wakati Will Smallbone alipiga juu ya lango kuikosesha Southampton penalti mbili, wakati upande wa Chelsea Mason Mount pekee alikosa.
  Waliofunga penalti za Chelsea ni Marcos Alonso, Callum Hudson-Odoi, Ben Chilwell na Reece James, wakati  Adam Armstrong, Shane Long na Oriol Romeu ndio waliofunga za Southampton.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHELSEA YAITOA SOUTHAMPTON KWA MATUTA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top