• HABARI MPYA

  Wednesday, October 13, 2021

  RONALDO APIGA HAT TRICK YA 10 URENO


  MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Cristiano Ronaldo jana amefunga mabao matatu kuiwezesha Ureno kuibuka na ushindi wa 5-0 dhidi ya Luxembourg katika mchezo wa Kundi A kufuzu Kombe la Dunia Barani Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Do Algarve Jijini São João da Venda.
  Ureno inafikisha pointi 16 baada ya ushindi huo katika mchezo wa sita, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi moja na Serbia ambayo hata hivyo imecheza mechi moja zaidi, wakati Luxembourg inabaki na pointi zake sita baada ya kucheza mechi sita pia.
  Katika mchezo huo wa Kundi A, Ronaldo alifunga mabao yake dakika za nane na 13 kwa penalti na 87, hiyo ikiwa hat-trick for yake ya 10 timu ya taifa, wakati mabao mengine ya Ureno yalifungwa na Bruno Fernandes dakika ya 17 na João Palhinha dakika ya 69.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RONALDO APIGA HAT TRICK YA 10 URENO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top