• HABARI MPYA

  Sunday, October 10, 2021

  MSUVA AING'ARISHA TAIFA STARS BENIN


  TANZANIA imefufua matumaini ya kufuzu kwenye Fainali za Kombe la Dunia mwakani Qatar baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Benin jioni ya leo Uwanja wa L' Amitié Jijini Cotonou.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee la Taifa Stars, mshambuliaji wa Wydad Athletics ya Morocco, Simon Happygod Msuva dakika ya sita tu akimchambua kipa Owalabi Franck Saturnin wa Valenciennes Ligue 2 ya Ufaransa baada ya kuwatoka mabeki wa Benin kufuatia kuanzishiwa mpira wa kurusha upande wa kulia wa Uwanja.
  Taifa Stars inayofundishwa na kocha Mdenmark, Kim Poulsen inafikisha pointi saba, sawa na Benin baada ya mechi tatu wakiwa mbele ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) yenye pointi tano na Madagascar ambayo haina pointi baada ya mechi tatu. 
  Madagascar wanawakaribisha DRC kuanzia Saa 1:00 usiku wa leo Uwanja wa Manispaa ya Mahamasina Jijini Antananarivo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MSUVA AING'ARISHA TAIFA STARS BENIN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top