• HABARI MPYA

  Saturday, October 30, 2021

  YANGA YAIKUNG'UTA AZAM FC 2-0


  MABAO ya washambuliaji Wakongo, Fiston Kalala Mayele na Jesus Ducapel Moloko yameipa Yanga SC ushindi wa 2-0 dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mayele alifunga bao la kwanza dakika ya 36 akimalizia kazi nzuri ya beki mzawa, Kibwana Shomari na Moloko akafunga dakika ya 73 akimalizia pasi ya mshambuliaji Mburkinabe, Yacouba Sogne.
  Kwa ushindi huo, Yanga SC inafikisha pointi 12 baada ya kucheza mechi nne na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi mbili zaidi ya Dodoma Jiji FC ambayo pia imecheza mechi moja zaidi.
  Azam FC yenyewe baada ya kichapo cha leo inabaki na pointi zake nne za mechi nne sasa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAIKUNG'UTA AZAM FC 2-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top