• HABARI MPYA

  Saturday, October 09, 2021

  TANZANITE YASONGA MBELE KOMBE LA DUNIA


  TIMU ya taifa ya Tanzania ya wasichana chini ya umri wa miaka 20 imefanikiwa kwenda Raundi ya Tatu ya michuano ya kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la mwakani baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ga Eritrea leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Mabao ya Tanzanite leo yamefungwa na Irene Kisisa na Protas Mbunda na kwa matokeo hayo, mabinti wa nchi ya Rais Samia Suluhu Hassan wanakwenda Raundi ya Tatu kwa ushindi wa jumla wa 5-0 kufuatia kuwachapa Eritrea 3-0 kwenye mechi ya kwanza Septemba 25 Jijini Asmara.
  Sasa Tanzania itamenyana na Burundi katika mfululizo wa kuwania tiketi ya fainali za Costa Rica Agosti mwakani. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TANZANITE YASONGA MBELE KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top