• HABARI MPYA

  Thursday, October 21, 2021

  AZAM FC WAIFUATA PYRAMIDS KUMALIZA KAZI CAIRO


  KIKOSI cha Azam FC kimeondoka Jumanne jioni kwenda Misri kwa ajili ya mchezo wa marudiano Raundi ya Pili Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji, Pyramids Jumamosi Uwanja wa Uwanja wa Jeshi la Anga wa Juni 30 Jijini Cairo.
  Azam inatatakiwa kushinda ugenini Jumamosi ili kusonga mbele baada ya kulazimishwa sare ya 0-0 Jumamosi Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.


  Mshindi wa jumla atamenyana na moja ya timu zitakazotolewa Ligi ya Mabingwa kuwania kucheza Hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC WAIFUATA PYRAMIDS KUMALIZA KAZI CAIRO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top