• HABARI MPYA

    Friday, October 15, 2021

    CAF YARUHUSU MASHABIKI MECHI ZA KLABU DAR


    SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF), limeruhusu mashabiki kuingia uwanjani kwenye mechi za klabu za Tanzania za michuano ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho.
    Wakati Biashara United watakuwa wenyeji wa Al Ahly Tripoli ya Libya jioni ya leo Uwanja wa Benjamin Mkapa, Azam FC watawaalika Pyramids ya Misri kesho Uwanja wa Azam Complex, Chamazi katika mechi za kwanza Raundi ya Pili Kombe la Shirikisho.
    Na mabingwa wa Tanzania, Simba SC wataanzia ugenini Jumapili dhidi ya Jwaneng Galaxy Jijini Gaborone, Botswana kabla ya kumalizia nyumbani wiki ijayo. 
    Ikumbukwe mechi za Raundi ya kwanza zote zilizozihusisha Azam, Biashara United na Yanga waliotolewa na Rivers United ya Nigeria katika Ligi ya Mabingwa hazikuwa na watazamaji kwa zuio la CAF ambayo ilizuia watazamaji hadi kwenye mechi za timu za Taifa nchini.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CAF YARUHUSU MASHABIKI MECHI ZA KLABU DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top