• HABARI MPYA

  Saturday, October 30, 2021

  CHELSEA YAICHAPA NEWCASTLE 3-0 ST JAMES


  TIMU ya Chelsea imeendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya England baada ya kuwachapa wenyeji, Newcastle United mabao 3-0 leo Uwanja wa St. James' Park .
  Mabao ya Chelsea leo yamefungwa na beki wa kimataifa wa England, Reece James mawili dakika ya 65 na 77 na kiungo Mtaliano mzaliwa wa Brazil, Jorge Luiz Frello Filho ‘Jorginho’ dakika ya 81.
  Kwa ushindi huo, The Blues inafikisha pointi 25 na kuendelea kuongoza ligi kwa pointi tatu zaidi ya Liverpool baada ya wote kucheza mechi 10, wakati Newcastle inabaki na pointi nne za mechi 10 pia katika nafasi ya 19.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHELSEA YAICHAPA NEWCASTLE 3-0 ST JAMES Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top