• HABARI MPYA

  Sunday, October 31, 2021

  SIMBA SC YALAZIMISHWA SARE 0-0 NA COASTAL


  MABINGWA watetezi, Simba SC wamelazimishwa sare ya bila kufungana na Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku wa leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Timu zote zilimaliza pungufu baada ya mchezaji mmoja kila upande kutolewa kwa kadi nyekundu, wakianza Coastal kumpoteza Benedictor Jacob Mwamlangwa dakika ya 29, kabla ya Simba kumpoteza beki wake Mkongo, Hennock Inonga Baka dakika ya 90.
  SIimba SC inafikisha pointi nane na Coastal imetimiza pointi tatu katika mchezo wa nne kila timu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YALAZIMISHWA SARE 0-0 NA COASTAL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top