• HABARI MPYA

  Saturday, October 23, 2021

  SARE ZA 1-1 MECHI ZOTE ZA LIGI KUU LEO


  MECHI zote mbili za Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo zimemalizika kwa sare ya 1-1 Namungo FC na KMC na Geita Gold na Mbeya City.
  Uwanja wa Ilulu mjini Lindi, Charles Ilamfya alianza kuifungia KMC dakika ya 30, kabla ya Shiza Kichuya kuisawazishia Namungo FC dakika ya 43 kwa penalti.
  Uwanja wa Nyankumbu, Juma Luizio alianza kuifungia Mbeya City dakika ya 45, kabla ya George Mpole kuwasawazishia wenyeji Geita dakika ya 57.
  Namungo inafikisha pointi tano, KMC pointi mbili sawa na Geita Gold na Mbeya City pointi sita baada ya timu zote kucheza mechi nne.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SARE ZA 1-1 MECHI ZOTE ZA LIGI KUU LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top