• HABARI MPYA

  Thursday, October 21, 2021

  TWIGA STARS WAENDA AFRIKA KUSINI KUIVAA TENA NAMIBIA


  TIMU ya taifa ya wanawake ya Tanzania, Twiga Stars imeondoka Dar es Salaam Jumatano usiku kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya mchezo wa marudiano na Namibia Jumamosi Uwanja wa Dobsonville Jijini Johannesburg Raundi ya Kwanza kufuzu AFCON ya mwakani Morocco.
  Twiga Stars imeondoka mara tu baada ya kuchapwa mabao 2-1 na Namibia nyumbani Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam jioni ya Jumatano.
  Mabao ya Namibia yote yalifungwa na kiungo mshambuliaji wa Sevilla ya Hispania, Zenatha Goeieman Coleman dakika ya 22 na 61, wakati bao pekee la Twiga Stars lilifungwa na kiungo wa JKT Queens, Stumai Abdallah Athumani dakika ya 41.


  Mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla kati ya Malawi na Zambia na atakayeshinda hapo amekata tiketi ya Morocco mwakani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TWIGA STARS WAENDA AFRIKA KUSINI KUIVAA TENA NAMIBIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top