• HABARI MPYA

  Thursday, October 07, 2021

  TAIFA STARS YACHAPWA 1-0 NA BENIN DAR


  TIMU ya taifa ya Tanzania imepoteza mechi ya kwanza ya kundi lake, J kufuzu Kombe la Dunia mwakani nchini Qatar baada ya kuchapwa 1-0 na Benin nyumbani Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam jioni ya leo.
  Bao pekee la Nguchiro leo limefungwa na mshambuliaji wa Brest ya Ligue 1 ya Ufaransa, Steve Michel Mounié dakika ya 71.
  Kwa matokeo hayo, Benin inajitanua kileleni ikifikisha pointi saba katika mechi tatu za mwanzo, ikifuatiwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), yenye pointi tano baada ya kuichapa Madagascar 2-0 leo Jijini Kinshasa.
  Taifa Stars inayobaki na pointi zake nne, sasa inaangukia nafasi ya tatu mbele ya vibonde, Madagascar waliopoteza mechi zote tatu za mwanzo, moja nyumbani dhidi ya Benin na mbili ugenini kwa DRC na Tanzania.
  Taifa Stars itasafiri kwenda Cotonou kwa ajili ya mchezo wa marudiano na Benin Jumapili, wakati DRC sasa inaifuata Madagascar.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TAIFA STARS YACHAPWA 1-0 NA BENIN DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top