• HABARI MPYA

  Saturday, October 23, 2021

  TWIGA STARS YATUPWA NJE KUFUZU AFCON


  TIMU ya taifa ya wanawake ya Tanzania, Twiga Stars imetupwa nje mbio za kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kuchapwa 3-2 na Namibia jioni ya leo Uwanja wa Dobsonville Jijini Johannesburg, Afrika Kusini.
  Mabao ya Namibia leo yamefungwa na kiungo mshambuliaji wa Sevilla ya Hispania, Zenatha Goeieman Coleman yote matatu, wakati ya Twiga Stars yamefungwa na kiungo mshambuliaji wa Chabab Atlas Khenifra ya Morocco Mwanahamisi Omary Shaluwa ’Gaucho’ na mshambuliaji wa Simba Queens, Opa Clement Sanga.
  Twiga Stars inatolewa kwa jumla ya mabao 5-3 baada ya kuchapwa 2-1 kwenye mchezo wa kwanza Jumatano Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.


  Siku hiyo mabao ya Namibia yote yalifungwa na Coleman, wakati bao pekee la Twiga Stars lilifungwa na kiungo wa JKT Queens, Stumai Abdallah Athumani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TWIGA STARS YATUPWA NJE KUFUZU AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top