• HABARI MPYA

    Monday, October 11, 2021

    UFARANSA BINGWA LIGI YA ULAYA


    UFARANSA imetwaa ubingwa wa Ligi ya Mataifa ya Ulaya baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Hispania usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Giuseppe Meazza Jijini Milan, Italia.
    Baada ya kipindi cha kwanza kumalizika bila mabao, dakika Mikel Oyarzabal alianza kuifungia Ufaransa dakika ya 64, kabla ya Karim Benzema kuisawazishia Ufaransa dakika moja baadaye na Kylian Mbappe kufunga la ushindi dakika ya 80.
    Mapema jioni ya jana katika mechi ya kusaka mshindi wa tatu, wenyeji Italia waliwachapa Ubelgiji 2-1 Uwanja wa Allianz Jijini Turin.
    Mabao ya Italia yalifungwa na Nicolo Barella dakika ya 46 na Domenico Berardi kwa penalti dakika ya 65, wakati la Ubelgiji lilifungwa na Charles De Ketelaere dakika ya 86.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: UFARANSA BINGWA LIGI YA ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top