TIKETI za mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika baina ya wenyeji, Simba SC na Jwaneng Galaxy ya Botswana utakaofanyika Jumapili wiki hii Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam tayari zimeanza kuuzwa.
Simba SC ilishinda 2-0 kwenye mchezo wa kwanza Jumapili iliyopita Uwanja wa Taifa Jijini Gaborone na kuelekea mchezo wa marudiano, wanaweza kununua tiketi kupitia mitandao ya simu.
0 comments:
Post a Comment