• HABARI MPYA

  Thursday, October 21, 2021

  MAN UNITED YASHINDA HADI KILELENI ULAYA


  TIMU ya Manchester United imetoka nyuma na kushinda 3-2 dhidi ya Atalanta katika mchezo wa Kundi F Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa Jumatano Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester.
  Atalanta ilitangulia kwa mabao ya Mario Pasalic dakika ya 15 na Merih Demiral dakika ya 28, kabla ya Man United kuzinduka kwa mabao ya Marcus Rashford dakika ya 53, Harry Maguire dakika ya 75 na Cristiano Ronaldo dakika ya 81.
  Kwa ushindi huo, Man United ya kocha Mnorway, Ole Gunnar Solskjaer inafikisha pointi sita na kupanda kileleni Kundi F ikizizidi pointi mbili kila moja, Atalanta na Villarreal, wakati Young Boys yenye pointi tatu inashika mkia baada ya mechi tatu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED YASHINDA HADI KILELENI ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top