• HABARI MPYA

    Tuesday, October 19, 2021

    ARSENAL YALAZIMISHWA SARE 2-2 NA PALACE


    WENYEJI, Arsenal jana wamelazimishwa sare ya 2-2 na Crystal Palace katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Emirates Jijini London.
    Mabao ya Crystal Palace inayofundishwa na mchezaji wa zamani wa Arsenal, Patrick Vieira yalifungwa na Christian Benteke dakika ya 50 na Odsonne Edouard dakika ya 73, wakati ya The Gunners yalifungwa na Nahodha, Pierre-Emerick Aubameyang dakika ya nane na Alexandre Lacazette dakika ya 90 na ushei.
    Arsenal inafikisha pointi 11 katika nafasi ya 12 na Crystal Palace inafikisha pointi nane katika nafasi ya 14 baada ya wote kucheza mechi nane.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ARSENAL YALAZIMISHWA SARE 2-2 NA PALACE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top