• HABARI MPYA

  Wednesday, October 13, 2021

  BODI YASOGEZA MBELE MECHI YA SIMBA


  BODI ya Ligi ya Tanzania (TPLB) imesogeza mbele mechi ya Ligi Kuu baina  ya mabingwa watetezi, Simba SC na Polisi Tanzania uliokuwa ufanyike Oktoba 20 hadi Oktoba 27.
  Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Almasi Kasongo amesema hatua hiyo imefuatia barua ya Simba SC wakiomba mechi hiyo isogezwe kwa sababu wamekosa ndege ya kuwahi kurejea nchini baada ya mechi yao ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, Jwaneng Galaxy FC Jijini Gaborone nchini Botswana Jumapili.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BODI YASOGEZA MBELE MECHI YA SIMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top