• HABARI MPYA

  Sunday, October 24, 2021

  SIMBA SC YATOLEWA LIGI YA MABINGWA

  MABINGWA wa Tanzania, Simba SC wametupwa nje ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuchapwa mabao 3-1 na Jwaneng Galaxy ya Botswana jioni ya leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Matokeo ya jumla yanakuwa 3-3 kufuatia Galaxy kufungwa 2-0 kwenye mchezo wa kwanza Jumapili iliyopita Jijini Gaborone, lakini Simba SC inatolewa kwa kuruhusu mabao zaidi nyumbani.
  Simba iliuanza vyema mchezo wa leo kwa bao la kiungo Mzambia, Rally Bwalya dakika ya 41, lakini Galaxy ikazinduka kipindi cha pili kwa mabao ya Rudath Wendell dakika ya 46 na 59 na Gape Mohutsiwa dakika ya 86.
  Wakati Galaxy inatinga hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa, Simba itakwenda kumenyana na moja ya timu za Kombe la Shirikisho kuwania kucheza hatua ya makundi pia ya michuano hiyo midogo ya CAF.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YATOLEWA LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top