• HABARI MPYA

  Wednesday, October 27, 2021

  BIASHARA YAICHAPA PRISONS 3-0 SUMBAWANGA


  TIMU ya Biashara United imewachakaza wenyeji, Tanzania Prisons mabao 3-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga mkoani Rukwa.
  Mabao ya Biashara United leo yamefungwa na mkongwe, Ramadhani Chombo ‘Redondo’ dakika ya 45, Dennis Nkane dakika ya 47 na Ambroce Awio dakika ya 90 na ushei.
  Ushindi huo wa kwanza katika mechi tatu baada ya kufungwa mechi moja na kutoa sare moja zote nyumbani, unaifanya Biashara United ifikishe pointi nne, wakati Tanzania Prisons wanafikisha mechi nne bila ushindi, wakifungwa kwa mara ya tatu na sare moja.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BIASHARA YAICHAPA PRISONS 3-0 SUMBAWANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top