• HABARI MPYA

  Jumamosi, Agosti 15, 2020

  MESSI NA BARCELONA YAKE TAABAN, WAPIGWA 8-2 NA BAYERN MUNCH

  Nyota wa Barcelona, Lionel Messi akitoka Uwanja wa Luz Jijini Lisbon, Ureno kinyonge baada ya timu yake kuchapwa 8-2 na Bayern Munich katika Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa usiku wa Ijumaa hicho kikiwa kipigo kikubwa zaidi kwa vigogo hao wa Hispania tangu mwaka 1940.
  Mabao ya FC Bayern Munich yamefungwa na Thomas Muller dakika ya nne na 31, Ivan Perisic dakika ya 21, Serge Gnabry dakika ya 27, Josh Kimmich dakika ya 63, Robert Lewandowski dakika ya 82 na Philippe Coutinho dakika ya 85 na 89, wakati ya Barcelona yamefungwa na David Alaba aliyejifunga dakika ya saba na Luis Suarez dakika ya 57.
  Sasa Bayern Munich itakutana na mshindi kati ya Manchester City na Olympique Lyon zinazomenyana Jumamosi katika Nusu Fainali Agosti 19 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MESSI NA BARCELONA YAKE TAABAN, WAPIGWA 8-2 NA BAYERN MUNCH Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top