• HABARI MPYA

  Jumatano, Novemba 06, 2019

  NDAYIRAGIJJE AENDELEA KUMKAUSHIA MANULA STARS, AITA 27 KUIVAA EQUATORIAL GUINEA WIKI IJAYO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KOCHA Mrundi wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Etienne Ndayiragijje ameendelea kumchunia kipa bora namba moja wa Simba SC, Aishi Salum Manula baada ya kumtenga katika kikosi cha awali cha wachezaji 27 kuelekea mechi na Equatorial Guinea Ijumaa ijayo.
  Taifa Stars watakuwa wenyeji wa Equatorial Guinea katika mchezo wa Kundi L kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2020 nchini Cameroon Ijumaa ya Novemba 15 kuanzia Saa 1:00 usiku Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
  Na leo Ndayiragijje kwa mara ya kwanza baada ya kuthibitishwa kuwa kocha Mkuu rasmi wa timu hiyo kufuatia kukaimu tangu Julai ametaja kikosi, ambacho pia kitatumika katika mchezo wa pili wa kufuzu AFCON dhidi ya Libya Jumanne ya Novemba 19.

  Aishi Salum Manula hayumo kwenye kikosi cha wachezaji 27 kwa ajili ya mechi na Equatorial Guinea Novemba 15

  Kikosi alichotaja Ndayiragijje kinaundwa na makipa; Juma Kaseja (KMC), Metacha Mnata (Yanga SC) na David Kisu (Gor Mahia).
  Mabeki; Salum Kimenya (Tanzania Prisons), Hassan Kessy (Nkana FC/Zambia), Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ (Simba SC), Gardiel Michael (Simba SC), Erasto Nyoni (Simba SC), Bakari Nondo (Coastal Union), Kelvin Yondan (Yanga SC) na Dickson Job (Mtibwa Sugar).
  Viungo; Jonas Mkude (Simba SC), Abdulaziz Makame (Yanga SC), Simon Msuva (Difaa El Jadida/Morocco), Eliuter Mpepo (Buildcon/Zambia), Iddi Suleiman (Azam FC), Salum Abubakar (Azam FC), Muzamil Yassin (Simba SC), Frank Domayo (Azam FC), Farid Mussa (Tenerife/Hispania), Hassan Dilunga (Simba SC),  
  Washambuliaji; Kelvin John (huru), Ayoub Lyanga (Coastal Union), )Ditram Nchimbi (Polisi Tanzania), Shaaban Iddi (Azam FC), Miraj Athumani ‘Madenge’ (Simba SC) na Nahodha Mbwana Samatta (KRC Genk/Ubelgiji).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NDAYIRAGIJJE AENDELEA KUMKAUSHIA MANULA STARS, AITA 27 KUIVAA EQUATORIAL GUINEA WIKI IJAYO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top