• HABARI MPYA

  Jumamosi, Novemba 30, 2019

  KOCHA JUMA MWAMBUSI ABWAGA MANYANGA MBEYA CITY, MOHAMED KIJUSO APEWA MIKOBA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KOCHA wa Mbeya City Juma Mwambusi (pichani) amejiuzulu kuifundisha timu hiyo kutokana na mwenendo usioridhisha kwenye ligi kuu msimu huu.
  Taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya James Kasusura imeeleza kuwa Kocha Mwambusi aliwasilisha barua ya kuomba kujiuzulu mnamo tarehe 26/11/2019 kwa maslahi mapana ya timu hiyo.
  Amesema kwa sasa bodi ya timu hiyo imekabidhi timu kwa kocha msaidizi Mohamed Kijuso wakati mchakato wa kumtafuta kocha mwingine ukiendelea.

  Hadi sasa timu hiyo ikiwa imecheza michezo 12 kwenye ligi kuu msimu huu, imeshinda mchezo mmoja, imetoka sare michezo mitano, imepoteza michezo sita, imefunga magoli manane, imefungwa mabao 19, ina pointi 8 na inakamata nafasi ya 19 juu ya Singida United ambao wanaburuza mkia wakiwa na pointi 7.
  “Bodi inamshukuru mwalimu Juma Mwambusi kwa mchango wake mkubwa kwa maendeleo ya timu na bado inahitaji ushauri na uzoefu wake katika tasnia ya michezo”, amesema Kasusura.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KOCHA JUMA MWAMBUSI ABWAGA MANYANGA MBEYA CITY, MOHAMED KIJUSO APEWA MIKOBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top