• HABARI MPYA

    Tuesday, November 12, 2019

    SAMATTA NA MSUVA WAWASILI TAIFA STARS KUIVAA EQUATORIAL GUINEA, MKUDE AENGULIWA KIKOSINI

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    NAHODHA wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars Mbwana Samatta amewasili usiku wa jana kujiunga na wenzake kwa maandalizi mchezo wa kufuzu AFCON 2021 dhidi ya Equatorial Guinea Ijumaa Novemba 15 Uwanja wa Taifa.
    Samatta anayecheza KRC Genk ya Belgium amewasili pamoja na winga Simon Msuva anayechezea Difaa Hassan El-Jadidi ya Morocco na wanatarajiwa kuiongoza Taifa Stars kwa mchezo huo dhidi ya Equatorial Guinea na mchezo utakaofuata siku 4 baadaye dhidi ya Libya utakaochezwa ugenini.
    Wachezaji wengine wanaocheza nje ya Tanzania wanaotarajia kuwasili leo usiku ni Farid Mussa anayecheza Tenerife ya Hispania na Simon Msuva anayecheza Difaa El Jadidi ya Morocco.
    Wachezaji wanaocheza nje ya Tanzania ambao tayari wameripoti Kambini ni David Kisu(Gor Mahia, Kenya), Ramadhan Kessy (Nkana, Zambia) na Eliuter Mpepo (Buildcon, Zambia)
    Taifa Stars tayari imeanza mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa ikipiga Kambi kwenye Hoteli ya Blue Saphire,barabara ya Pugu.
    Mchezo dhidi ya Equatorial Guinea utachezwa saa 1 usiku Uwanja wa Taifa Ijumaa Novemba 15. Kiingilio kwenye mchezo huo ni shilingi 3,000 mzunguko,5,000 VIP B na C.
    Wakati huo huo: Kiungo wa Simba SC Jonas Mkude ameenguliwa kwenye kikosi baada ya kuomba ruhusa kutokana na matatizo ya kifamilia.
    Kocha Mrundi, Etienne Ndayiragijje amesema kwamba baada ya kuombwa na Mkude amemruhusu kuendelea kushughulikia matatizo yake ya kifamilia na hatahusika kwenye mechi zote mbili zijazo za Taifa Stars. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SAMATTA NA MSUVA WAWASILI TAIFA STARS KUIVAA EQUATORIAL GUINEA, MKUDE AENGULIWA KIKOSINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top