• HABARI MPYA

  Alhamisi, Novemba 07, 2019

  SIMBA SC YAVUTWA MKIA NYUMBANI NA TANZANIA PRISONS, YALAZIMISHWA SARE 0-0 UHURU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MABINGWA watetezi, Simba SC leo wamelazimishwa sare ya bila kufungana na Tanzania Prisons ya Mbeya katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.
  Sare hiyo inawaongezea pointi moja Wekundu wa Msimbazi na kufikisha 22 baada ya kucheza mechi tisa, wakiendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi nne zaidi ya Lipuli FC wanaofuatia nafasi ya pili kwa pointi zao 18 baada ya kucheza mechi 10.
  Tanzania Prisons wenyewe wanafikisha poinri 16 katika mchezo wa 10 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya nne sasa wakiizidi kwa wastani wa mabao tu Namungo FC ya Lindi inayoangukia nafasi ya tano.

  Katika mchezo wa leo, refa wa kike Jonesia Rukyaa kutoka Kagera kama kawaida yake alikuwa mkali kwa wachezaji na akatoa jumla ya kadi za njano tano, nne kwa Tanzania Prisons peke yao.
  Walioonywa kwa kadi za njano ni Adilly Buha dakika ya 43, Ezekia Mwashilindi dakika ya 45, Nurdin Chona dakika ya 54 na Jeremia Kisubi dakika ya 76 kwa upande wa Tanzania Prisons na upande wa Simba SC ni Jonas Mkude pekee dakika ya 68.
  Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Erasto Nyoni, Pascal Wawa, Jonas Mkude, Clatous Chama/Hassan Dilunga dk80, Meddie Kagere, Ibrahim Ajibu/ Deo Kanda dk56 na Francis Kahata/Rashid Juma dk70.
  Tanzania Prisona: Jeremiah Kusubi, Michael Ismail, Laurian Mpalile, Vedastus Mwihambi, Nurdin Chona, Adilly Buha, Salum Kimenya/Cleophace Mkandala dk62, Ezekia Mwashilindi, Samson Mbangula/ Lambert Sabiyanka dk90+7, Ismail Aziz na Benjamin Asukile/ Jeremia Juma dk46.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAVUTWA MKIA NYUMBANI NA TANZANIA PRISONS, YALAZIMISHWA SARE 0-0 UHURU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top