• HABARI MPYA

  Jumatatu, Novemba 25, 2019

  YANGA SC YAUNDA KAMATI MPYA YA MASHINDANO MWENYEKITI YULE YULE GUMBO

  Na Saada Akida, DAR ES SALAAM
  MJUMBE wa Kamati ya Utendaji ya Yanga SC, Rodgers Gumbo amerejeshewa madaraka ya Uenyekiti wa Kamati Mashindano kiasi cha wiki mbili tangu apokonywe.
  Novemba 7, mwaka huu Kamati ya Utendaji ya Yanga SC iliivunja Kamati ya Mashindano ya klabu iliyokuwa chini ya Mwenyekiti, Gumbo na Makamu wake, Saad Mkhiji.
  Wajumbe walikuwa ni Hamad  Islam, Makaga, Leonard Bugomola, Ally Kamtande, Said Side, Bonnah Kamoli, Sudi Mlinda, Tom Lukuvi, Martin Mwampashi, Hamza Jabir Mahoka, Edward Urio, Kawina Konde, Abednego Ainea na Edwin Muhagama.
  Mhandisi Deo Mutta (katikati) ameteuliwa tena kuwa Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya Yanga

  Lakini leo Afisa Habari na Mawasiliano wa klabu, Hassan Bumbuli ametangaza Kamati mpya ya Mashindano, Gumba akiwa Mwenyekiti na Makamu wake, Hamad Ismail.
  Wajumbe ni Salum Mkemi, Hassan Hussein, Beda Tindwa, Thobiaa Lingalangala, Edward Urio, Max Komba, Yusuphed Mhandeni, Yanga Makanga, Adonis Bitegeko na Wahandisi Hersi Said, Heriel Mhulo, Isaac Usaka na Deo Mutta.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA SC YAUNDA KAMATI MPYA YA MASHINDANO MWENYEKITI YULE YULE GUMBO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top