• HABARI MPYA

  Jumanne, Novemba 12, 2019

  KAMPUNI YA SBL MDHAMINI MKUU MASHINDANO YA GOFU YA WAITARA 2019 YATAKAYOFANYIKA LUGALO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  JUMLA ya wachezaji 120 wa gofu kutoka sehemu mbali mbali hapa nchini, wanatarajiwa kuchuana vikali mwishoni mwa wiki katika mashindano ya Waitara Gofu ya mwaka 2019 yanayodhaminiwa na kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL).
  Mashindano hayo ya siku moja, yatafanyika siku ya Jumamosi katika viwanja vya Gofu vya Lugalo jijini Dar es Salaam.
  Akitangaza udhamini huo jijini Dar es Salaam, Meneja masoko wa SBL Anitha Msangi aliwaambia waandishi wa habari kuwa udhamini wa SBL kwenye mashindano hayo maarufu, unalenga kuendeza mchezo wa gofu hapa nchini.
  Meneja masoko wa SBL Anitha Msangi akipeana mkono wa pongeza na Mwenyekiti wa klabu ya  Lugalo Gofu Brigedia Generali Mstaafu, Michael Luwongo mara baada ya kutangaza udhamini wa kampuni ya bia ya Serengeti kwenye mashindano ya Waitara Gofu ya mwaka 2019. Wengine ni Nahodha wa Lugalo, Kapt. Japhet Masai (kulia) na Afisa Utawala wa klabu hiyo Luteni. Samwel Mosha.
  Meneja masoko wa SBL Anitha Msangi akizungumza na waandishi wa habari leo. Wengine ni Brigedia Generali Mstaafu, Michael Luwongo (katikati) na Nahodha wa Lugalo , Kapt. Japhet Masai

  “Kampuni ya SBL kupitia bia yake pendwa ya Serengeti Premium Lager inayofuraha kuwa mdhamini mkuu wa mashindano ya gofu ya Waitara ya mwaka huu. Udhamini huu unaonyesha nia yetu ya dhati ya kuendeleza michezo hapa nchini,” alisema Anitha.
  Kupitia bia ya Serengeti Premium Lager, kampuni ya SBL ni mdhamini mkuu wa Timu ya Taifa, Taifa Stars Serengeti na pia inadhamini ligi ya taifa ya wanawake kupitia bia yake ya Serengeti Lite.
  Kwa upande wake, mwenyekiti wa klabu ya Gofu ya Lugalo Brigedia Jenerali mstaafu Michael Luwongo aliishukuru kampuni ya SBL kwa udhamini huo na kuyataka makampuni na taasisi nyoingine kuiga mfano wa SBL na kujitokeza kusaidia michezo wa gofu nchini.
  “Tunaishukuru sana kampuni ya SBL kwa mchango wake kwenye kusaidia maendeleo ya michezo hapa nchini na hususani gofu. SBL imekuwa mdhamini mkubwa wa mashindano haya,” alisema.
  Mashindano ya Waitara Golf hufanyikja kila mwaka yakilenga kutambua mchango wa Genelrali mstaafu George Waitara aliyekuwa mkuu wa majeshi kwa kuanzisha klabu ya golf ya Lugalo.
  Klabu ya Golf ya Lugalo ilianza mwaka 2006 kutokana na mchango mkubwa wa Waitara ambo pia uliendelezwa na Generali Davis Mwamunyange ambaye alimfuatia baada ya kustaafu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KAMPUNI YA SBL MDHAMINI MKUU MASHINDANO YA GOFU YA WAITARA 2019 YATAKAYOFANYIKA LUGALO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top