• HABARI MPYA

  Jumatano, Novemba 20, 2019

  KILIMANJARO QUEENS YAKAMILISHA MECHI ZA MAKUNDI KIBABE CHALLENGE, YAIPIGA ZENJI WIKI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TANZANIA Bara imekamilisha mechi zake za Kundi A michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge Wanawake kwa ushindi wa 7-0 dhidi ya Zanzibar jioni ya leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Matokeo hayo yanamaanisha Kilimanjaro Queens inamaliza kama kinara wa Kundi A kwa pointi zake tisa na mabao 20 ya kufunga, ikiwa haijafungwa hata bao moja hivyo kwenda Nusu Fainali kibabe na itakutana na mshindi wa pili wa Kundi B.
  Mabao ya Kilimanjaro Queens inayofundishwa na kocha Bakari Nyundo Shime anayesaidiwa na Edna Lema ‘Mourinho’ leo yamefungwa na Deonisia Daniel Minja dakika za 26, 56, Diana Lucas dakika ya 31, Philomena Daniel dakika ya 70, Asha Rashid ‘Mwalala’ dakika ya 84 na 86 na Anastazia Anthony Katunzi dakika ya 90.


  Zanzibar inamalizia mkiani katika kundi hilo baada ya kufungwa mechi zote, nyingine 5-0 kila mechi dhidi ya Burundi na Sudan Kusini. Queens, mabingwa mara mbili mfululizo wa michuano hiyo, waliipiga 9-0 Sudan Kusini na 5-0 Burundi katika mechi zake mb ili za mwanzo.
  Mechi za mwisho za Kundi B zitafanyika kesho, Djibouti ikimenyana na Ethiopia kuanzia Saa 8:00 mchana na Kenya dhidi ya Uganda kuanzia Saa 10:30 jioni. Kenya na Uganda kila moja ina pointi sita baada ya zote kuzifunga Djibouti na Ethiopia.
  Kikosi cha Tanzania Bara kilikuwa; Zubeda Mgunda, Asha Saada, Fatuma Issa, Fatuma Khatib ‘Foe’, Anastazia Anthony, Eva Wailes, Janeth Christopher, Diana Lucas, Deonisia Minja, Philomena Daniel na Mwanahamisi Omary ‘Gaucho’. 
  Zanzibar; Hajra Abdallah, Warda Abdulhakim, Mary Charles, Mwanajuma Abdallah, Aziza Mwadini, Hawa Ali, Neema Suleiman, Sabahi Hashim, Neema Machano, Nasrini Mohamed na Siwazuri Mrisho.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KILIMANJARO QUEENS YAKAMILISHA MECHI ZA MAKUNDI KIBABE CHALLENGE, YAIPIGA ZENJI WIKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top