• HABARI MPYA

  Ijumaa, Novemba 08, 2019

  AZAM FC YAILAZA 2-1 BIASHARA UNITED YA MARA MECHI YA LIGI KUU TANZANIA BARA LEO CHAMAZI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Azam FC imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Biashara United katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku wa leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam.
  Ushindi huo wa kwanza chini ya Mromania Aristica Cioaba tangu arejeshwe unaifanya Azam FC ifikishe pointi 13 baada ya kucheza mechi saba na kupanda hadi nafasi ya 11 kutoka ya 14.
  Mabao ya Azam FC katika mchezo wa leo yamefungwa na kiungo Idd Suleiman ‘Nado’ dakika ya pili akimalizia pasi ya Mshambuliaji Mzimbabwe, Donald Ngoma na beki Mganda, Nicolas Wadada dakika ya 23 akimalizia pasi ya mshambuliaji Mzambia Obrey Chirwa.

  Bao pekee la Biashara United ya Mara leo limefungwa na mshambuliiaji wake hodari, Inocent Edwin dakika ya 35 na kwa kupoteza mechi hiyo timu hiyo inabaki nafasi ya 17 katika ligi ya timu 20 ikiwa na pointi nane baada ya kucheza mechi 10.
  Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, YANGA SC imeshinda 1-0 dhidi ya wenyeji, Ndanda FC 1-0 bao pekee nyota wa Rwanda Partrick Sibomana dakika ya 76 Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara. 
  Nayo Kagera Sugar imeendelea kufanya vizuri baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, KMC Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.
  Mabao ya Kagera Sugar inayofundishwa na Nahodha wa zamani wa Taifa Stars, Mecky Mexime yamefungwa na viugno Awesu Awesu kwa penlati dakkika ya 25 na Peter Mwalyanzi dakika ya 48, wakati la KMC ya kocha Mganda, Jackson Mayanja limefungwa na Serge Nogues dakika ya 86.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM FC YAILAZA 2-1 BIASHARA UNITED YA MARA MECHI YA LIGI KUU TANZANIA BARA LEO CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top