• HABARI MPYA

  Jumatano, Novemba 13, 2019

  MAMBO YAZIDI KUIVA KUELEKEA CECAFA CHALLENGE YA WANAWAKE, WAGENI ZAIDI WAWASILI DAR

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU mbalimbali zimeanza kuwasili Tanzania kuelekea kwenye mashindano ya Cecafa kwa Wanawake yatakayoanza Novemba 16 hadi 25 mwaka huu Jijini Dar es Salaam.
  Tayari timu za Burundi na Djibout zimetua jana Jumanne na kuelekea kwenye Hoteli zilizopangiwa.
  Leo timu za Kenya na Ethiopia zinataraji kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
  Uganda wenyewe wanatarajia kuingia Kesho mchana sawa na Zanzibar huku pia tukiitarajia timu ya Sudan Kusini.
  Wenyeji Tanzania Bara 'Kilimanjaro Queens' mabingwa watetezi tayari wapo Kambini wakiendelea kujifua.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAMBO YAZIDI KUIVA KUELEKEA CECAFA CHALLENGE YA WANAWAKE, WAGENI ZAIDI WAWASILI DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top