• HABARI MPYA

  Jumatatu, Novemba 11, 2019

  YANGA SC YACHAPWA 1-0 MASASI, YAMTANGAZA RASMI LUHAGO KUWA KATIBU MKUU WAKE MPYA

  Na Mwandishi Wetu, MASASI
  TIMU ya Yanga SC leo imechapwa 1-0 na wenyeji, Mkuti Market FC ya Masasi bao pekee la assan Mtepeto dakika ya 28 katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Boma, Masasi mkoani Mtwara. 
  Mchezo huo ulikuja siku moja tu baada Yanga kuichapa 5-0  Komabini ya Nanyumbu 5-0 katika mchezo wake wa kwanza wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Halmashauri ya wilaya Nanyumbo mkoani Mtwara.
  Jana, mabao ya Yanga yalifungwa na mshambuliaji Adam Stanley aliyefunga matatu dakika za  19, 45 na 58, beki Muharami Issa ‘Marcelo’ moja kwa penalti dakika ya 35 na lingine mshambuliaji James Wilson dakika ya 89.
  Huu unakuwa mchezo wa tatu Yanga kucheza Mtwara, baada ya kushinda 1-0 dhidi ya wenyeji, Ndanda FC katika mechi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Nangwanda SIjaona mjini Mtwara Ijumaa, bao pekee la Mnyarwanda Patrick Sibomana.
  Kikosi cha Yanga SC leo kilikuwa; Ramadhani Kabwili, Vincent Paschal, Muharami Issa ‘Marcelo’, Cleophas Sospeter/Saad Kassim dk60, Mustafa Suleiman, Said Juma ‘Makapu’, Gustapha Simon/Said Kwangala dk80, Lukengelo Majimoto, Adam Stanley, Raphael Daud/Best Eliud dk60, Jaffar Mohamed. 
  Wakati huo huo: Uongozi wa Yanga SC umemthibitisha David Luhago kuwa Katibu Mkuu mpya wa klabu hiyo, akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Charles Boniface Mkwasa ambaye kwa sasa ni Kaimu Kocha Mkuu wa klabu.
  Taarifa iliyotolewa leo na Afisa Habari wa Yanga SC, Hassan Bumbuli imesema kwamba uteuzi wa Luhago aliyewahi kuwa Mjumbe wa Kamati mbalimbali za Yanga katika vipindi tofauti, umefanywa na Kamati ya Utendaji ya klabu chini ya Mwenyekiti wake, Dk. Mshindo Msolla.
  Katika kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja tangu kuondoka madarakani aliyekuwa Katibu wa timu hiyo Charles Boniface Mkwasa, nafasi hiyo imekaimiwa na viongozi watatu tofauti ambao ni Omar Kaya, Dismas Ten na Thabit Kandoro aliyekaimu nafasi hiyo kwa siku 11 tu tangu Novemba 1, mwaka huu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA SC YACHAPWA 1-0 MASASI, YAMTANGAZA RASMI LUHAGO KUWA KATIBU MKUU WAKE MPYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top