• HABARI MPYA

  Jumapili, Novemba 10, 2019

  YANGA SC YASHINDA MECHI YA PILI MFULULIZO CHINI YA MKWASA, YAICHAPA 5-0 NANYUMBU

  Na Mwandishi Wetu, NANYUMBU
  KIKOSI cha Yanga SC leo kimepata ushindi wa pili mfululizo chini ya kocha mpya na wa muda, Charles Boniface Mkwasa baada ya kuwachapa wenyeji, Komabini ya Nanyumbu 5-0 katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Halmashauri ya wilaya Nanyumbo mkoani Mtwara.
  Baada ya kufukuzwa kocha Mkongo, Mwinyi Zahera mapema wiki hii, Mkwasa aliiongoza Yanga kushinda 1-0 dhidi ya wenyeji, Ndanda FC katika mechi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Nangwanda SIjaona mjini Mtwara Ijumaa.
  Na baada ya mchezo huo Yanga leo imecheza mechi ya kirafiki ikitumia sehemu kubwa ya wachezaji wa timu yake ya vijana chini ya umri wa miaka 20, maarufu kama Yanga B.

  Mshambuliaji Adam Stanley alifunga mabao matatu dakika za  19, 45 na 58, beki Muharami Issa ‘Marcelo’ moja kwa penalti dakika ya 35 na lingine mshambuliaji James Wilson dakika ya 89.
  Mara tu baada ya mchezo huo, kikosi cha Yanga kikaunganisha safari hadi Masasi ambako kesho jioni watacheza mechi nyingine ya kirafiki dhidi ya wenyeji, Jangwa Uwanja wa Boma.
  Kikosi cha Yanga SC leo kilikuwa; Ramadhani Kabwili, Vincent Paschal, Muharami Issa ‘Marcelo’, Cleophas Sospeter, Mustafa Suleiman, Said Juma ‘Makapu’, Gustapha Simon/Said Kwangala dk80, Lukengelo Majimoto, Adam Stanley, Raphael Daud/James Julius dk60, Jaffar Mohamed/Best Eliud dk60. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA SC YASHINDA MECHI YA PILI MFULULIZO CHINI YA MKWASA, YAICHAPA 5-0 NANYUMBU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top