• HABARI MPYA

  Jumatano, Novemba 20, 2019

  MOURINHO ASAINI MKATABWA WA HADI 2023 TOTTENHAM

  KLABU ya Tottenham imemtangaza Mreno Jose Mourinho kuwa kocha wake mpya kwa mkataba wa hadi mwishoni mwa msimu wa 2022-2023.
  Mourinho, ambaye atakuwa analipwa karibu mara mbili ya mtangulizi wake , Mauricio Pochettino mshahara wa Pauni Milioni 15 kwa mwaka, amesema: "Nina furaha kujiunga na klabu kubwa kama hii na yenye mashabiki wenye mashamsham. Ubora wa vyote, kikosi na akademi vimenivutia. Kufanya kazi na wachezaji hao ndicho kilichonivutia,".
  Hapana shaka Mourinho ni kocha babu kubwa akiwa ameshinda mataji 25 katika historia yake, wakati Tottenham ilitwaa taji la mwisho mwaka 2008, Kombe la Ligi.

  Mreno Jose Mourinho amesaini mkataba wa hadi mwishoni mwa msimu wa 2022-2023 kujiunga na Spurs 

  Mreno huyo ameshinda mataji matatu ya Ligi Kuu ya England katika awamu zake mbili za kufundisha Chelsea na ametwaa mataji mawili ya Ligi ya Mabingwa, moja akiwa na Porto na moja Inter Milan, ambako alitwaa mataji matatu msimu mmoja.
  Ameshinda mataji mawili ya Ligi za nchi akiwa na Porto na Inter, sambamba na Real Madrid taji la La Liga mwaka 2012 akikusanya pointi 100, akiizidi pointi tisa Barcekona iliyokuwa chini ya kocha Pep Guardiola. 
  Lakini mara ya mwisho hakuondoka vizuri kazini alipokuwa Manchester United licha ya kuipa mataji ya Europa League na Kombe la League msimu wa 2016-17 kutokana na kufanya vibaya kwenye Ligi Kuu.
  Pochettino alifukuzwa Tottenham usiku wa Jumanne baada ya miaka mitano kazini kufuatia mwanzo mbaya wa msimu wa Ligi Kuu. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MOURINHO ASAINI MKATABWA WA HADI 2023 TOTTENHAM Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top