• HABARI MPYA

  Jumatatu, Novemba 11, 2019

  SAMATTA ACHEZA HADI MWISHO KRC GENK YACHAPWA 2-0 NYUMBANI KATIKA LIGI YA UBELGIJI

  Na Mwandishi Wetu, GENK
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta jana amecheza kwa dakika zote 90, klabu yake KRC Genk ikichapwa 2-0 nyumbani na KAA Gent katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk.
  Mabao yaliyoizamisha Genk, mabingwa watetezi wa Ligi ya Ubelgiji jana yalifungwa na washambuliaji Mbelgiji Laurent Depoitre dakika ya tatu na Mcanada Jonathan David dakika ya 47.
  Kipigo hicho kinazidi kupunguza matumaini ya Genk kutetea ubingwa, kwani sasa inazidiwa pointi 13 na vinara Club Brugge, wakati Gent sasa inafikisha pointi 28 ikipanda nafasi ya pili, ikiizidi pointi moja tu Standard Liege inayofuatia katika nafasi ya tatu. 
   
  Samatta jana amecheza mechi ya ya 174 jumla kwenye mashindano yote tangu ajiunge na KRC Genk Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) akiwa amefunga mabao 69.
  Katika ligi ya Ubelgiji pekee hiyo inakuwa mechi ya 136 akiwa amefunga mabao 53, kwenye Kombe la Ubelgiji amecheza mechi tisa na kufunga mabao mawili, katika Super Cup mechi moja, Ligi ya Mabingwa Ulaya mechi nne mabao mawili na Europa League mechi 24 na mabao 14.
  Kikosi cha KRC Genk kilikuwa: Coucke, Maehle, Cuesta/Bongonda dk55, Lucumi, Dewaest, De Norre, Berge, Heynen, Hrosovsky/Ito dk63, Onuachu/Ndongala dk77 na Samatta.
  KAA Gent: Kaminski, Ngadeu, Owusu, Yaremchuk/Kvilitaia dk82, Bezus/Dejaegere dk55, Castro-Montes, Mohammadi, David, Kums, Depoitre/Mbayo dk90+2 na Plastun.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SAMATTA ACHEZA HADI MWISHO KRC GENK YACHAPWA 2-0 NYUMBANI KATIKA LIGI YA UBELGIJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top