• HABARI MPYA

  Alhamisi, Novemba 21, 2019

  KILIMANJARO QUEENS KUMENYANA NA UGANDA KATIKA NUSU FAINALI YA CECAFA CHALLENGE

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TANZANIA Bara itamenyana na Uganda katika Nusu ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge Wanawake Jumamosi Saa 10: 00 jioni Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Nusu Fanal nyingine ya michuano hiyo ya tat utu ya CECAFA Challenge wakubwa upande wa wanawake itatangula Saa 8:00 mchana kati ya Burundi na Kenya hapo hapo Azam Complex, Jumamosi.
  Fainali ya michuano hiyo itafanyika Jumatatu Saa 10:00 jioni ikitanguliwa na mchezo wa kusaka mshindi wa tatu. 
  Kilimanjaro Queens imetinga Nusu Fainali baada ya kuongoza Kundi A kufuatia kushinda mechi zake zote za kundi hilo, ikiichapa 7-0 Zanzibar, 9-0 Sudan Kusini na 5-0 Burundi katika mechi zake tatu za mwanzo hivyo kuongoza kundi hilo kwa pointi zake tisa na mabao 20 ya kufunga, ikiwa haijafungwa hata bao moja hivyo kwenda Nusu Fainali kibabe.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KILIMANJARO QUEENS KUMENYANA NA UGANDA KATIKA NUSU FAINALI YA CECAFA CHALLENGE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top