• HABARI MPYA

  Jumamosi, Novemba 30, 2019

  SIMBA SC YAACHANA NA AUSSEMS, KITAMBI APEWA TIMU HADI ATAKAPOPATIKANA KOCHA MPYA

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Simba SC imetangaza rasmi kuachana na kocha wake, Patrick Winand J. Aussems baada ya beki huyo wa zamani wa kimataifa wa Ubelgiji kushindwa kufikia malengo ya mwajiri wake na kwa sasa timu itakuwa chini ya Kocha Msaidizi, Dennis Kitambi hadi hapo atakapopatikana kocha mpya.
  Katika taarifa yake kwa vyombo vya Habari leo, Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Senzo Mbatha Mazingisa raia wa Afrika Kusini amesema kwamba wameachana na Aussems kwa sababu ameshindwa kutekeleza majukumu yake kwa viwango na malengo aliyokubaliana na klabu kwenye mkataba wake wa ajira ikiwemo kufika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
  “Pamoja na jitihada za dhati za Bodi kumpa ushirikiano ndugu Patrick Winand J. Aussems hata baada ya kutolewa kwenye mashindano ya klabu binga Afrika, bado ameendelea kuisimamia bila kujali malengo ya Simba kujenga timu yenye ari na mafanikio, nidhamu na ushindani kwenye mashindano ya ndani nan je ya nchi,”imesema taarifa ya Mazingisa.


  Simba SC imeaachana na Patrick Aussems baada ya miezi 16 tangu achukue nafasi ya Mfaransa, Pierre Lechantre

  Uamuzi huo wa Bodi unakuja siku tano tu baada ya Aussems kusimamishwa kwa sababu za utovu wa nidhamu na utetezi wake alioutoa kwenye kikao cha Kamati ya Nidhamu juzi haukuwa na mashiko baada ya kuondoka kwenye kituo cha kazi bila ruhusa.
  Mazingisa amesema kwamba Aussems alikataa kuiambia Kamati ya Nidhamu alipokwenda na sababu za kwenda bila ruhusa.
  Aussems alijiunga na Simba SC Julai 19 mwaka jana akitokea timu ya taifa ya Nepal, akichukua nafasi ya Mfaransa, Pierre Lechantre aliyeondoka Mei. 
  Katika kipindi miezi 16 ya klabu, Aussems ameiongoza Simba kucheza mechi 91, ikishinda 61, ikifungwa 13 na sare 17, ndani yake akiipa mataji matatu, ubingwa wa Ligi Kuu na Ngao ya Jamii mawili pamoja na kufikisha Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa msimu uliopita.
  Hadi anaondolewa, Simba SC inaongoza Ligi Kuu ikiwa na pointi zake 25 baada ya kucheza mechi 10, ikifuatiwa kwa mbali na Kagera Sugar yenye pointi 24 za mechi 13.
  Aussems inaachana na Kocha mwenye uzoefu wa kufundisha timu kadhaa Asia na Ulaya – lakini amewahi kufundisha KSA ya Cameroon na AC Leopards ya Dolisie nchini Kongo, hizo zikiwa timu pekee za Afrika.
  Aussems alianza kama mchezaji wa kwao, akichezea klabu za RCS Vise (1974–1981), Standard Liege (1981–1988), K.A.A. Gent (1988–1989), R.F.C. Seraing (1989–1990) na ES Troyes AC ya Ufaransa kuanzia mwaka 1990 hadi 1993, ambayo ilikuwa timu yake ya kwanza kufundisha akianza kama kocha mchezaji mwaka 1992.
  Mwaka 1995 alienda kufundisha SS Saint-Louisienne hadi 1999 alipohamia Capricorne Saint-Pierre hadi 2002 alipokwenda Stade Beaucairois hadi 2003 alipojiunga na Stade de Reims zote za Ufaransa hadi mwaka 2004 alipokuja Afrika kufundisha KSA ya Cameroon hadi mwaka 2006 aliporejea Ufaransa kufundisha SCO Angers.
  Timu nyingine alizofundisha ni Evian Thonon Gaillard F.C. ya Ufaransa pia kuanzia 2009 hadi 2011 alikwenda China kufundisha Shenzhen Ruby (2011) na Chengdu Blades kuanzia 2012 hadi 2013 aliporudi Afrika kufundisha AC Leopards hadi mwaka 2015 alipokwenda kufundisha timu ya taifa ya Nepal.
  Aliyekuwa Kocha Msaidizi, Dennis Kitambi ataongoza timu hadi hapo atakapopatikana kocha mpya

  REKODI YA PATRICK J AUSSEMS SIMBA SC
  1. Simba SC 1-1 F.C.E KSAIFA (ya Palestina, kirafiki ziara ya Uturuki)
  2. Simba SC 3-1 MC Oujder (ya Morocco, Kirafiki ziara ya Uturuki)
  3. Simba SC1-1 Asante Kotoko (ya Ghana, Kirafiki Taifa)
  4. Simba SC 0-0 Namungo FC (Kirafiki Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa, Lindi)
  5. Simba SC 2-1 Arusha United (Kirafiki Uwanja wa S.A. Abeid, Arusha)
  6. Simba SC 2-1 Mtibwa Sugar (Ngao ya Jamii Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza)
  7. Simba SC 1-0 Tanzania Prisons (Ligi Kuu Taifa)
  8. Simba SC 2-0 Mbeya City (Ligi Kuu Taifa)
  9. Simba SC 4-2 AFC Leopards (Kirafiki Taifa)
  10. Simba SC 0-0 Ndanda FC (Ligi Kuu Mtwara)
  11. Simba SC 0-1 Mbao FC (Ligi Kuu Mwanza)
  12. Simba SC 3-1 Mwadui FC (Ligi Kuu Shinyanga)
  13. Simba SC 0-0 Yanga SC (Ligi Kuu Taifa)
  14. Simba SC 2-1 African Lyon (Ligi Kuu Taifa)
  15. Simba SC 3-0 Stand United (Ligi Kuu Taifa)
  16. Simba SC 5-1 Alliance FC (Ligi Kuu Taifa)
  17. Simba SC 5-0 Ruvu Shooting FC (Ligi Kuu Taifa)
  18. Simba SC 2-0 JKT Tanzania (Ligi Kuu Mkwakwani)
  19. Simba SC 0-0 Big Bullets (Kirafiki Uwanja wa Taifa)
  20. Simba SC 0-0 Lipuli FC (Ligi Kuu Uwanja wa Taifa)
  21. Simba SC 4-1 Mbabane Swallows (Ligi ya Mabingwa Afrika Taifa)
  22. Simba SC 4-0 Mbabane Swallows (Ligi ya Mabingwa Afrika Manzini) 
  23. Simba SC 1-2 Nkana FC (Ligi ya Mabingwa Afrika Kitwe) 
  24. Simba SC 2-1 KMC (Ligi Kuu Uwanja wa Taifa)
  25. Simba SC 3-1 Nkana FC (Ligi ya Mabingwa Afrika Taifa) 
  26. Simba SC 3-0 Singida United (Ligi Kuu Uwanja wa Taifa)
  27. Simba SC 4-1 Chipukizi United (Kombe la Mapinduzi, Zanzibar)
  28. Simba SC 1-0 KMKM (Kombe la Mapinduzi, Zanzibar)
  29. Simba SC 1-0 Mlandege (Kombe la Mapinduzi, Zanzibar)
  30. Simba SC 0-0 (3-1 penalti) Malindi SC (Alikuwa Dar na timu A, Kombe la Mapinduzi, Zanzibar)
  31. Simba SC 3-0 JS Saoura (Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika Taifa)
  32. Simba SC 1-2 Azam FC (Alibaki Dar, Fainali Kombe la Mapinduzi, Zanzibar)
  33. Simba SC 0-5 AS Vita (Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika Kinshasa)
  34. Simba SC 2-1 AFC Leopards (SportPesa Super Cup Taifa)
  35. Simba SC 1-2 Bandari FC (SportPesa Super Cup Taifa)
  36. Simba SC 0-0 (Penalti 5-3) Mbao FC (SportPesa Super Cup Taifa)
  37. Simba SC 0-5 Al Ahly (Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika Cairo)
  38. Simba SC 3-0 Mwadui FC (Ligi Kuu Taifa)
  39. Simba SC 1-0 Al Ahly (Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika Dar)
  40. Simba SC 1-0 Simba SC (Ligi Kuu Taifa)
  41. Simba SC 3-0 African Lyon (Ligi Kuu Sheikh Amri Abeid)
  42. Simba SC 3-1 Azam FC (Ligi Kuu Taifa)
  43. Simba SC 3-1 Lipuli FC (Ligi Kuu Samora)
  44. Simba SC 2-0 Stand United (Ligi Kuu Kambarage)
  45. Simba SC 0-2 JS Saoura (Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika Bechar)
  46. Simba SC 2-1 AS Vita (Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika Dar)
  47. Simba SC 2-0 Ruvu Shooting (Ligi Kuu Taifa)
  48. Simba SC 2-0 Ruvu Shooting (Ligi Kuu Taifa)
  49. Simba SC 3-0 Mbao FC (Ligi Kuu Taifa)
  50. Simba SC 0-0 TP Mazembe (Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Afrika Dar)
  51. Simba SC 1-4 TP Mazembe (Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Afrika Lubumbashi)
  52. Simba SC 2-1 Coastal Union (Ligi Kuu Mkwakwani, Tanga)
  53. Simba SC 1-2 Kagera Sugar (Ligi Kuu Kaitaba, Bukoba)
  54. Simba SC 2-0 Alliance FC (Ligi Kuu Kirumba, Mwanza)
  55. Simba SC 2-1 KMC (Ligi Kuu Kirumba, Mwanza)
  56. Simba SC 2-0 Biashara United (Ligi Kuu Musoma, Mara)
  57. Simba SC 1-0 JKT Tanzania (Ligi Kuu, Uhuru)
  58. Simba SC 2-1 Mbeya City (Ligi Kuu, Sokoine)
  59. Simba SC 1-0 Tanzania Prisons (Ligi Kuu, Sokoine)
  60. Simba SC 8-1 Coastal Union (Ligi Kuu, Uhuru)
  61. Simba SC 0-1 Kagera Sugar (Ligi Kuu, Uhuru)
  62. Simba SC 0-0 Azam FC (Ligi Kuu, Uhuru)
  63. Simba SC 3-0 Mtibwa Sugar (Ligi Kuu, Uhuru)
  64. Simba SC 2-0 Ndanda FC (Ligi Kuu, Uhuru)
  65. Simba SC 2-0 Singida United (Ligi Kuu, Namfua)
  66. Simba SC 4-5 Sevilla (Kirafiki Taifa)
  67. Simba SC 1-1 Biashara United (Ligi Kuu Taifa)
  68. Simba SC 0-0 Biashara United (Ligi Kuu Jamhuri, Morogoro) 
  69. Simba SC 4-0 Orbit Tvet (Rusternburg)  
  70. Simba SC 4-1 Platnums Stars (Kirafiki kambini Rusternburg)  
  71. Simba SC 1-1 Township Rollers (Kirafiki kambini Rusternburg)  
  72. Simba SC 1-1 Orlando Pirates (Kirafiki kambini Johannesburg)  
  73. Simba SC 3-1 Power Dynamos (Kirafiki Taifa Simba Day)
  74. Simba SC 0-0 UD Songo (Ligi ya Mabingwa Beira)
  75. Simba SC 4-2 Azam FC (Ngao ya Jamii Taifa)
  76. Simba SC 1-1 UD Songo (Ligi ya Mabingwa Taifa)
  77. Simba SC 3-1 JKT Tanzania (Ligi Kuu Uhuru)
  78. Simba SC 2-1 Mtibwa Sugar (Ligi Kuu Uhuru)
  79. Simba SC 3-0 Kagera Sugar (Ligi Kuu Kaitaba)
  80. Simba SC 2-0 Biashara United (Ligi Kuu Musoma)
  81. Simba SC 1-0 Bandari FC (Kirafiki Taifa)
  82. Simba SC 1-0 Mashujaa FC (Kirafiki Kigoma)
  83. Simba SC 0-0 Aigle Noir FC (Kirafiki Kigoma)
  84. Simba SC 1-0 Azam FC (Ligi Kuu Taifa)
  85. Simba SC 1-0 Singida United (Ligi Kuu Arusha)
  86. Simba SC 0-1 Mwadui FC (Ligi Kuu Shinyanga)
  87. Simba SC 4-0 Mbeya City (Ligi Kuu Uhuru)
  88. Simba SC 0-0 Tanzania Prisons (Ligi Kuu Uhuru)
  89. Simba SC 1-2 KMC (KIrafiki Chamazi)
  90. Simba SC 1-0 JKT Tanzania (Kirafiki Chamazi)
  91. Simba SC 3-0 Ruvu Shooting (Ligi Kuu Uhuru)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAACHANA NA AUSSEMS, KITAMBI APEWA TIMU HADI ATAKAPOPATIKANA KOCHA MPYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top