• HABARI MPYA

  Jumamosi, Novemba 23, 2019

  MISRI WABEBA TAJI LA AFCON U-23 BAADA YA KUIPIGA IVORY COAST 2-1

  WENYEJI, Misri wamefanikiwa kutwaa Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa 23, (AFCON  U-23) baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Ivory Coast usiku wa jana katika fainali iliyodumu kw adakika 120 Uwanja wa Kimataifa wa Cairo.
  Hilo linakuwa taji la kwanza kabisa kwa Misri la michuano hiyo mipya barani ya kusaka wawakilishi wa kwenye Michezo ya Olimpoiki ya mwakani, Tokyo 2020.
  Karim El Iraky alianza kuifungia Misri dakika ya 37, kabla ya Aboubakar Doumbia kuisawazishia Ivory Coast ikiwa imebaki dakika moja mchezo kumalizika. 

  Lakini Nahodha Ramadan Sobhy akawafungia wenyeji bao la ushindi dakika ya 116 kikosi cha Olimpiki cha Mafarao kikitwaa ubingwa kimtindo, huo ukiwa ushindi wao wa tano kwenye michuano hiyo.
  Misri inaungana na mabingwa wawili wa awali wa michuano hiyo, Gabon mwaka 2011 na Nigeria 2015 kwenye orodha ya washindi wa taji hilo.
  Ramadan Sobhy aliondoka na tuzo mbili baada ya mchezo huo, Mchezaji Bora wa Mechi na Mchezaji Bora wa Mashindano, wakati Kipa Bora ni Mohamed Sobhy, Mfungaji Bora ni Mostafa Mohamed, wote wa Misri, ambayo kama timu imeshinda Tuzo ya Soka ya kiungwana.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MISRI WABEBA TAJI LA AFCON U-23 BAADA YA KUIPIGA IVORY COAST 2-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top