• HABARI MPYA

  Jumamosi, Novemba 23, 2019

  AZAM FC YAICHAPA MBAO 1-0 KIRUMBA, SINGIDA UNITED YAIPIGA MBEYA CITY 1-0 SOKOINE

  Na Mwandshi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Azam FC imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Mbao FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.
  Bao pekee la Azam FC katika mchezo wa leo limefungwa na beki Mghana, Yakubu Mohamed dakika ya 15 akimalizia kazi nzuri ya mshambuliaji Mzimbabwe, Donald Dombo Ngoma.
  Kwa ushindi huo, Azam FC iliyo chini ya kocha Mromania, Aristica Cioaba inafikisha pointi 16 katika mchezo wa nane na kupanda hadi nafasi ya sita kutoka ya 13.


  Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Singida United wameibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Mbeya City bao pekee la Emmanuel Manyanda dakika ya 85 Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
  Biashara United ikalazimishwa sare ya 0-0 na Mtibwa Sugar Uwanja wa Karume mjini Musoma mkoani Mara, wakati mabao ya Miraji Athumani dakika ya 40 na 75 na Tairone Santos dakika ya 47 yakaipa Simba SC ushindi wa 3-0 dhidi ya Ruvu Shooting Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM FC YAICHAPA MBAO 1-0 KIRUMBA, SINGIDA UNITED YAIPIGA MBEYA CITY 1-0 SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top