• HABARI MPYA

  Jumamosi, Novemba 16, 2019

  SIMBA SC YACHEZEA KICHAPO KWA KMC, YAPIGWA 2-1 KATIKA MECHI YA KIRAFIKI LEO CHAMAZI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Simba SC leo imechapwa 2-1 na wapinzani wao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, KMC katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam.
  Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Mussa Gabriel aliyesaidiwa na Innocent Mwalutanile na Hassan Buhanza baada ya dakika 45 ngumu za kipindi cha kwanza, milango ikafunguka kipindi cha pili. 
  Mabao ya KMC yamefungwa na kiungo Kenny Ally Mwambungu dakika ya 58 na 68, wakati la Simba limefungwa na Ibrahim Ajibu kwa penalti dakika ya 90 na ushei baada ya kiungo Mbrazil, Gerson Fraga ‘Viera’ kuangushwa kwenye boksi. 

  KMC ilikuwa inacheza mechi ya kwanza tangu imefukuze kocha wake Mganda, Jackson Mayanga na leo ikiwa chini ya kaimu kocha Mkuu, Mrage Kabange imepata ushindi. 
  Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Beno Kakolanya, Shomari Kapombe, Kenedy Juma, Santos Tairone, Haruna Shamte, Gerson Fraga, Said Ndemla, Francis Kahata, Deo Kanda, Ibrahim Ajibu na Wilker Da Silva.
  KMC; Dennis Richard, Boniphace Maganga, Ally Ramadhani, Abdallah Mfuko, Ismail Gambo, Rayman Mgungila, Serge Tape, Kenny Ally, Hassan Kabunda, Mohamed Samatta na Rehani Kibingu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA SC YACHEZEA KICHAPO KWA KMC, YAPIGWA 2-1 KATIKA MECHI YA KIRAFIKI LEO CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top