• HABARI MPYA

  Ijumaa, Novemba 29, 2019

  MANULA ATEULIWA KIKOSI CHA KILIMANJARO STARS PAMOJA NA KASEJA KWA AJILI YA CHALLENGE

  Na Asha Said, DAR ES SALAAM
  KIPA namba moja wa timu ya Simba, Aishi Manula amerejeshwa kwenye kikosi cha timu ya taifa, baada ya jana kutajwa kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) kitachoshiriki michuano ya CECAFA Senior Challenge nchini Uganda .
  Chini ya kocha wa sasa Etienne Ndayirajige, Manula aliitwa mara moja pekee katika mechi za awali kufuzu CHAN, lakini kuumia kukamuweka pembeni, hakujumuishwa tena Katika mtanange mingine ikiwamo kufuzu Makundi ya awali Kombe la Dunia pamoja na Afcon mechi za awali.
  Kikosi kamili cha Kilimanjaro Stars ni; Makipa; Aishi Manula (Simba SC), Juma Kaseja (KMC), Matecha Mnata (Yanga SC) na David Kisu (Gor Mahia/Kenya), 
  Mabeki; Juma Abdul (Yanga), Nickson Kibabage (Difaa Hassan El –Jadid/Morocco), Mwaita Gereza (Kagera Sugar), Kelvin Yondani (Yanga SC), Salum Kimenya (Tanzania Prisons), Bakari Mwamnyeto (Coastal Union), Mohamed Hussein (Simba SC), Gardiel Michael (Simba SC) na Abdulimajid Mangalo (Biashara United).
  Viungo; Zawadi Mauya (Kagera Sugar), Yussuf Mhilu (Kagera Sugar), Jonas Mkude, Muzamil Yassin (Simba SC), Hassan Diliunga (Simba SC), Cleophace Mkandala (Tanzania Prisons), Salum Abubakar ‘Sure Boy’ (Azam FC), Iddi Suleiman ‘Nado’ (Azam FC) na Freddy Tangalu (Lipuli FC).
  Washambuliaji; Paul Nonga (Lipuli FC), Miraji Athuman ‘Madenge’ (Simba SC), Shaaban Iddi Chilunda (Azam FC), Ditram Nchimbi (Polisi Tanzania), Kelvin John (Football House), Eliud Ambokile (TP Mazembe/DRC), Eliuther Mpepo (Bulidcon/Zambia) na Lucas Kikoti (Namungo FC).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MANULA ATEULIWA KIKOSI CHA KILIMANJARO STARS PAMOJA NA KASEJA KWA AJILI YA CHALLENGE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top